MWINJILISTI KKKT: KRISMAS SIO KUJIREMBA, KUNYWA NA KULA PEKEE

Описание к видео MWINJILISTI KKKT: KRISMAS SIO KUJIREMBA, KUNYWA NA KULA PEKEE

Moshi. Mwinjilisti wa Usharika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), mtaa wa Idstein, Usharika wa Pasua mjini Moshi,Godfrey Maro amewataka waumini wa Kanisa hilo na Watanzania kutoichukulia Sikukuu ya Krismas kuwa ni siku ya kunywa na kula pekee.

Akihubiri katika mkesha wa sikukuu ya Krismas, mwinjilisti Marro, amesema furaha ya siku hiyo si kwenye mavazi, kusuka nywele mpya au kula na kunywa, bali furaha hiyo iwe ni kwa sababu Yesu Kristu amezaliwa.

Kauli ya mwinjilisti Maro imekuja wakati mji wa Moshi na maeneo ya uchagani na wilaya nyingine za mkoa wa Kilimanjaro, ukiwa umefurika wageni wenyeji ambao wana utamaduni wa kurejea mkoani humo kila mwisho wa mwaka, kusherehekea sikukuu za Krismas na mwaka mpya.

Video na Ombeni Daniel.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке