MCHEKESHAJI MKWELE MBELE YA RC CHALAMILA "SISI HATUUZI BANGI TUNALESENI, HATUNA KISASI NA NYINYI"

Описание к видео MCHEKESHAJI MKWELE MBELE YA RC CHALAMILA "SISI HATUUZI BANGI TUNALESENI, HATUNA KISASI NA NYINYI"

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amekutana na wamiliki wa Bars, Night Clubs na GroceryJijini Dar es salaam

Akiongea na wamiliki hao RC Chalamila amesema maeneo hayo ya starehe yanabeba watu wengi ni fursa kubwa ya ajira kwa vijana na husaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla lakini pia ni hatari kama biashara zitaendeshwa pasipo kuzingatia misingi ya amani, hivyo ni vizuri kujiepushe kuwa vichaka vya waovu, vibaka na majambazi hivyo ni wajibu wetu sote kumuunga mkono Mhe Raisi Dkt Samia S. Hassan kwa kulipa kodi bila shuruti kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi na watu wake.

Aidha Chalamila amewataka wamiliki hao kufanya kazi kutokana na leseni zao zinavyowataka huku mchakato wa kurekebisha sheria ya muda inayo wataka kufungua biashara saa 10 jioni mpaka saa 5 usiku kwa siku za kazi na siku za mwisho wa juma kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 6 usiku unaendelea.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке