"OCD ONDOKA NA MWENYEKITI" SAKATA LA NYUMBA ZAIDI YA 30 KUVUNJWA, RC CHALAMILA AAGIZA WAKAMATWE

Описание к видео "OCD ONDOKA NA MWENYEKITI" SAKATA LA NYUMBA ZAIDI YA 30 KUVUNJWA, RC CHALAMILA AAGIZA WAKAMATWE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila baada ya kuwasikiliza waathirika wa mgogoro wanaodai kuvunjiwa nyumba zaidi ya 30 amemuagiza OCD na TAKUKURU kumkamata Mwenyekiti wa mtaa wa Majoe ili aweze kuhojiwa ni watu gani wamefanya uhalifu huo eneo la Majoe Wilaya ya Ilala

" haiwezekani watu wanakuja kubomoa nyumba usiku alafu awajulikani na mwenyekiti yupo hili halikubaliki" Alisema RC Chalamila

Vilevile RC Chalamila amemtaka OCD kuwasaka na kuwakamata wote waliojihusisha na tukio hilo, apeleleze kwa kina ajue ni akina nani, hatua itakayofuata ni atakuja tena na vyombo vyake pamoja na timu ya wataalam wanasheria na Wataalam wa Ardhi ili kupata ufumbuzi wa mzizi wa mgogoro huo

Aidha RC Chalamila ameagiza eneo hilo kuanzia sasa lilindwe ili Isitokee uharibifu au ubomoaji mwingine wa aina yeyote, ambapo amesistiza kitendo kilichofanyika halivumiliki pia kina chafua taswira ya Jeshi la polisi, Kinamchafua, Rais na Chama cha mapinduzi kwa ujumla.

RC Chalamila ameyasema hayo alipotembelea eneo hilo na kujionea nyumba zilizo bomolewa na watu ambao hawafahamiki kwa kuwa uhalifu huo umekua ukifanyika nyakati za usiku.

Kwa upande wa Mhe Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amesema alifika katika eneo hilo na kujionea nyumba zilizo bomolewa ambazo ni zaidi ya 30 na wamiliki wa nyumba hizo hadi sasa wamekua wakihangaika kutokana na kukosa makazi.

Mwisho RC Chalamila amesema hatua aliyoichukua ni ya awali ili apate pa kuanzia na ijulikane wazi hatengui wala kuingilia hukumu ya mahakama.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке