BENKI KUU YAZUIA KAMPUNI HIZI KUTOA MIKOPO

Описание к видео BENKI KUU YAZUIA KAMPUNI HIZI KUTOA MIKOPO

DAR ES SALAAM: BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa orodha ya Majukwaa na Programu Tumizi ‘Applications 69 zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka BOT.

Katika taarifa iliyotoa kwa umma, BOT imesema majukwaa na programu hizo hazijakidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 walioutoa Agosti 27 mwaka huu (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2 Microfinance Service Providers, 2024).

“Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao,” imeeleza taarifa hiyo.Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo:   / spotileo-176.  .
HabariLeo:   / habarileo  
DailyNews:   / dailynewstz  

INSTAGRAM;
HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig...
SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid...

TWITTER;
Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09

Комментарии

Информация по комментариям в разработке