MAMA MARIA NI MAMA YETU- Kwaya ya Mt Mikaeli Malaika Mkuu Chang'ombe DSM(Mtunzi Aloyce Kipangula)

Описание к видео MAMA MARIA NI MAMA YETU- Kwaya ya Mt Mikaeli Malaika Mkuu Chang'ombe DSM(Mtunzi Aloyce Kipangula)

MAMA MARIA NI MAMA YETU. By Aloyce Kipangula. KWAYA Mt MIKAELI PAROKIA YA CHANG'OMBE JIMBO KUU KATOLIKI DAR ES SALAAM

Mama Maria ni Mama yetu, Mama maria ni mama yetu kwa sababu ameunganika na Yesu mwanaye katika kutukomboa x 2

1 Mama huyu Bikira Maria, yeye ndiye Eva mpya mnyenyekevu na mwenye huruma, mama wa Neema,
Kupitia kwa mama Maria, tulimpata Mkombozi aliyekuja kutukomboa utumwani mwa shetani hivyo mama Maria........

2 Yesu alipomwona mama yake, na mwanafunzi wake Yohane alimwambia Mama tazama, Huyo ndiye mwanao,
Kisha akamwambia Yohane, mtazame mama yako Yohane akamchukua Maria akae nyumbani kwake hivyo Mama....

3 Na katika Harusi ya kana walitindikiwa divai Maria akamwambia mwanaye, hawana divai,
Yesu akamtii mama yake, akawarejeshea furaha kwa kuwa aliyageuza maji yakawa divai hivyo...

4 Hata katika nyakati zetu, tunapungukiwa tunatindikiwa tunamuhitaji yesu katika maisha,
Tumwendee mama Maria, atatuombea kwa Yesu na Yesu atamtii mama yake atatujalia hivyo..

Комментарии

Информация по комментариям в разработке