AIC Chang'ombe Choir (CVC) - USIKU WA MANANE (Official Live Video)

Описание к видео AIC Chang'ombe Choir (CVC) - USIKU WA MANANE (Official Live Video)

#USIKU WA MANANE ni wimbo wa kumi na mbili katika IBADA YA MOYO WA SHUKRANI iliyofanyika 10 NOV, 2023 katika kanisa la AICT Chang'ombe, Sokota Temeke Dar es salaam.
Ndani ya wimbo huu AIC Chang'ombe Choir tunamshukuru Mungu kwa baraka zake alizotukirimia kwa zaidi ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa kwaya yetu.
Tunaamini wimbo huu utaenda kukusaidia kuisikia sauti ya MUNGU. MUNGU AKUBARIKI.

LYRICS

Kuanguka usiku wa manane kuna mateso usiku wa manane
Kuinuka usiku wa manane kuna neema usiku wa manane

Usiku wa manane usiku mtulivu (Shetani)
Anavyoutumia kuleta huzuni (mateso)
Wagonjwa wengi sana huzidiwa (usiku wa manane)
Na tena wengi wao hufariki (usiku wa manane)
Na hata wizi mwingi hufanyika (usiku wa manane)
Na mauaji mengi ya kutisha (usiku wa manane)

eeh (usiku wa manane)
eh iyee (usiku wa manane)
Uuuh (usiku wa manane)

Usiku wa manane usiku wa pekee (shetani)
Anavoutumia kuchafua hewa (mateso)
Vikao vya wachawi hufanyika (usiku wa manane)
Tena ni wakati wa mazindiko (usiku wa manane)
Makaburini nako matambiko (usiku wa manane)
Uchafu mwingi sana hufanyika (usiku wa manane)

Usiku wa manane usiku mtulivu (Jehova)
Anavyoutumia kuleta amani (furaha)
Kuzama kwa maombi ukimwita (usiku wa manane)
Ukitafuta uso wake Bwana (usiku wa manane)
Utaiona mbingu iko wazi (usiku wa manane)
Uwepo wake Bwana umejaa (usiku wa manane)

Usiku wa manane usiku wa ajabu (JEHOVA)
Huzungumza nae kila amwitae (furaha)
Na huo ndio muda wa kutubu (usiku wa manane)
Kujitakasa mbele zake MUNGU (usiku wa manane)
Na kumweleza kikusumbuacho (usiku wa manane)
Majibu ya maombi utapata (usiku wa manane)

Paulo na Sila walimwona BWANA
Walimwona (usiku wa manane)
Walikuta (milango ya gereza)
Iko wazi (usiku wa manane)

Wanawali watano wenye busara
Walimwona (usiku wa manane)
Bwana harusi (usiku wa manane)
Walimwona (usiku wa manane)

Usiku wa manane usiku wa Baraka
Usiku wa manane ni usiku wa Sifa
Usiku wa manane usiku wa Neema
Usiku wa manane usiku wa Ushindi


Special Thanks
AICT CHANG'OMBE CHURCH
Mch. Dr Joseph Mayala Mitinje

CREDITS.
Song writer - Barthrolomew Magulu
AICT Chang'ombe Church
AIC Chang'ombe Choir (CVC)

MUSIC DEPARTMENT
Music Team - Benjamin Makolobela (MD,MAIN KEYS)
Elisha Gurlaty (AUX 1)
Elia Mahuna (AUX 3)
Onesmo Peter (AUX 2)
Emmanuel Yusuph (BASS)
Daniel (LEAD GUITAR)
Mayala Bubele (TRUMPET)
Charles Stenson (TROMBONE)
Meshack Wilson (TROMBONE)
Eliya Makaya (ALTO SAX)
Raphael Luhende (ALTO SAX)
Samson Mathew (DRUMS)

Video production - CVC Media
Audio Mixing & Mastering Engineer - Tamie Bimha
Sound System, Backline, Lights, Stage - Haddypro Campany Limited
Project Manager - Dr.Elidady Msangi Ejazz01 Music Pro

Комментарии

Информация по комментариям в разработке