MIGUU ILIYOHAMISHWA (II) - PASTOR SUNBELLA KYANDO

Описание к видео MIGUU ILIYOHAMISHWA (II) - PASTOR SUNBELLA KYANDO

2 Samweli 22:34
[34]Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu;
Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.

Kulungu ni mnyama ambaye anaweza kukimbia kwa speed sana.Anaposema "huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu" maana yake amenipa uwezo wa kwenda kwa speed kama ambavyo kulungu ana speed(Kasi).Kwa maana nyingine kabla hajafanya iwe kama ya kulungu (Kasi) kuna namna ilikuwa mwanzo,ilikuwa inaenda mwendo wa polepole sana.Hii ni lugha ya picha,maana yake huyu mtu mambo yake mwanzoni yalikuwa yanaenda polepole sana,kila akifanya kitu hadi kije kifanikiwe kinakuwa kimechukua muda mrefu sana na ametumia nguvu nyingi sana.Na hawa watu wapo wengi,hakuna kitu ambacho kinaleta matokeo katika muda sahihi,ni lazima kichelewe.
Lakini Biblia inaendelea kusema "Na kunisimamisha mahali pangu pa juu"
- Hapa mahali pa juu ni sehemu kabisa anayojua kuwa ni yake,Mungu amempa na ndio maana anasema "pangu".Huyu mtu alikuwa anajua kuna sehemu anatakiwa kuwepo japo hakuwepo hapo kwa wakati huo,ndio maana ndani yako unajua kabisa ulipo sipo unapotakiwa kuwa,maisha unayoishi siyo unayotakiwa kuyaishi..kuna picha unaiona ndani yako ya mahali unapotakiwa kuwa.Kama huyu mtu Mungu alimuweka mahali pa juu maana yake mwanzoni alikuwa chini,na utajua kuwa upo chini kutokana na matokeo yanayoonekana kwenye maisha yako,matokeo huwa hayajifichi.

Kitu cha kwanza adui alifanya kwa huyu mtu ni kuondoa speed(Kasi) kwenye miguu yake,na Mungu alipokuja jambo la kwanza ni kufungua kwanza miguu yake.Mungu akakufungue miguu yako na akurudishe kwenye njia yako uliyohamishwa.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке