Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo || Mjadala wa Somo 12 | 19/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile

Описание к видео Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo || Mjadala wa Somo 12 | 19/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile

Somo la Juma Hili
Yn. 18:33—19:5; Yn. 19:17-22; Yn. 19:25—27; Lk. 2:34, 35; Yn. 20:1-18; 1 Kor. 15:12—20.

Fungu la Kukariri

“Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu” (#Yohana 18:37#).
Kusulubiwa na kufufuka kwa Yesu ndiyo kilele cha Yohana. Sura kumi za kwanza zinahusu takribani miaka mitatu na nusu; sura ya 11-20, kinyume chake, inashughulika na takribani juma moja hadi mawili.

Injili nne zinawasilisha kifo cha Yesu kwa njia tofauti tofauti. Ingawa masimulizi yao yanapatana, kila mwandishi anakazia mambo makuu yenye umuhimu hasa kwa mada za Injili yake. Mathayo anasisitiza utimilifu wa Maandiko; Marko anasisitiza ufanani kati ya ubatizo wa Yesu na msalaba; na Luka anajikita kwa msalaba kama uponyaji na wokovu (kisa cha mwizi msalabani).

Lakini Yohana anawasilisha msalaba kama kutawazwa kwa Yesu, hasa kuhusiana na wazo la saa, ambayo inayorejelewa mara nyingi katika kitabu (Yn. 7:30, Yn. 8:20, Yn. 12:27). Wazo hili la kutawazwa ni taswira ya kushangaza kwa kuwa kusulubiwa kulikuwa njia ya kufedhehesha na ya aibu zaidi ambayo Warumi walitumia. Tofauti hii inaelekeza katika taswira ya kushangaza kabisa ambayo Yohana anawasilisha: Yesu anakufa kwa aibu, lakini, wakati huo huo, ni kutawazwa kwake kwa utukufu kama Mwokozi.

Jifunze somo la juma hili unapojiandaa kwa ajili ya Sabato ya Desemba 21.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке