Swali Lisilo Sahihi na Jibu la Yesu: Kudumu Kumtaza Yesu || Somo 13 || 23/ 12/ 2024

Описание к видео Swali Lisilo Sahihi na Jibu la Yesu: Kudumu Kumtaza Yesu || Somo 13 || 23/ 12/ 2024

Soma Yohana 21:20-22. Ni swali gani lilimwelekeza Petro katika njia isiyo sahihi? Yesu aliinyoshaje njia?

Yesu alikuwa ametoka tu kumrejesha Petro kwenye huduma na kumwambia, “Nifuate” (Yn. 21:19). Pengine ilikuwa ni kumfuata Yesu kimwili kwenda ufukweni. Na hiyo ni kwa sababu Petro anageuka na kumwona Yohana akimfuata Yesu pia, naye anauliza kuhusu Yohana. “ 'Bwana, na huyu je?' ” (Yn. 21:21).

Katika kumrejesha Petro katika huduma, Yesu alikuwa ametabiri namna ya kifo cha Petro (Yn. 21:18). Inaonekana Petro alikuwa na shauku ya kutaka kujua kifo cha Yohana pia. Badala yake, Yesu anaelekeza usikivu wa Petro katika suala la kumfuata, ila kuwa na wasiwasi kuhusu kitakachompata mwanafunzi mwingine.

Soma Yohana 21:23-25. Ni kwa namna gani kauli ya Yesu haikueleweka? Mtume Yohana alisahihishaje huo uelewa wenye makosa?

Watu walielewa visivyo kile Yesu alichomaanisha aliposema, “Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe unifuate mimi! ” (Yn. 21:22). Walifikiri ilimaanisha kwamba Yesu angerudi kabla ya Yohana kufa. Kadiri muda ulivyopita na Yohana akawa mzee, ingekuwa zahama ikiwa angekufa (ambalo, bila shaka, alikufa) na Yesu alikuwa hajarudi. Yohana anasahihisha uelewa huu mbaya kwa kuonesha kwamba lilikuwa jambo la mapenzi ya Yesu, si unabii wa kile ambacho kingetukia.

Wazo la kukaza fikra kwa Yesu, badala ya watu wengine, ni mwongozo wenye nguvu katika sehemu iliyosalia ya somo juma hili. Yesu, na Yesu pekee, ndiye Mwokozi wetu. Kwa hakika watu watakukatisha tamaa, huenda hata kukuumiza pia.

Kweli tutakazojifunza kwa siku ya Jumanne hadi Alhamisi zitaendeleza mada ya kuelewa Neno la Mungu, kwa lengo la kumjua na kumfuata Yesu, ambaye peke yake ndiye anapaswa kuwa Bwana na Kiongozi wetu bila kujali msaada, ushauri na mwongozo ambavyo wengine wanaweza kutupatia.

Ni mara ngapi watu wengine, ambao ungewatazama na kupendezwa nao wamekukatisha tamaa? Ni masomo gani ingawa ni magumu, ulijifunza kutokana na uzoefu huo?

Комментарии

Информация по комментариям в разработке