HOTUBA KAMILI YA RAIS MAGUFULI AKIWA TARIME - 07/09/2018

Описание к видео HOTUBA KAMILI YA RAIS MAGUFULI AKIWA TARIME - 07/09/2018

Ni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo Septemba 7, 2018 kwenye Chuo cha Ualimu Tarime ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Mara.

Katika kuhitimisha ziara yake mkoa wa Mara, Rais Magufuli amehutubia mkutano wa hadhara Mjini Tarime na kuwahakikishia wananchi wa mji huo kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwahudumia wananchi bila kuwabagua.

Katika hotuba hii Rais Maguli ameeleza sababu ya kumuondoa kwenye nafasi yake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola, amekemea vitendo vya rushwa na ubadhirifu ndani ya CCM, pia amemkaribisha CCM mbunge wa CHADEMA Ester Matiko.

Amesema kwamba kwa Tarime serikali imetenga shilingi Bilioni 14 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji, imeanza ujenzi wa barabara ya Tarime – Mugumu kwa kiwango cha lami, imetoa shilingi milioni 400 za ujenzi wa kituo cha afya, inatoa fedha za elimu bila malipo kila mwezi na inaendelea kusambaza umeme kwa vijiji vyote visivyo na umeme.

Rais Magufuli amezungumzia uwekezaji wa shamba la miwa na kiwanda cha sukari katika wilaya ya Tarime, na kueleza kuwa Serikali itafanya uchambuzi wa kina kabla ya kuridhia mradi huo huku akiwataka viongozi wa Mkoa na Wilaya kuondoa tofauti zao.

Kwa wilaya jirani ya Rorya Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo kutafuta fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga hospitali.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке