HOTUBA YA RAIS MAGUFULI AKIWA UKEREWE - 04/09/2018

Описание к видео HOTUBA YA RAIS MAGUFULI AKIWA UKEREWE - 04/09/2018

Rais Magufuli ambaye yuko ziarani mkoani Mwanza amezungumza na wananchi wa Nansio wilayani Ukerewe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja Ukuta Mmoja ambapo amesema Serikali imedhamiria kutekeleza dhamira ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ya kukiendeleza kisiwa cha Ukerewe kwa kuhakikisha inajenga miundombinu ya barabara ya uhakika, inaimarisha huduma za elimu, maji, umeme na afya, na hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali katika utekelezaji wa dhamira hiyo.

Ameongeza kuwa sambamba na juhudi hizo Serikali ya Awamu ya Tano imechukua hatua madhubuti za kusimamia rasilimali za umma ikiwemo kudhibiti wizi, ufisadi na rushwa pamoja na kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo kuongeza uzalishaji wa umeme utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa gharama nafuu kwa ajili ya maendeleo ya viwanda.

Kuhusu uvuvi, Rais Magufuli amempongeza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kwa juhudi zake za kukabiliana na uvuvi haramu ambazo sasa zimeanza kuzaa matunda kwa samaki kuongezeka katika ziwa Victoria huku akibainisha kuwa uvuvi haramu uliokuwepo umesababisha viwanda vingi vya samaki kufa, ajira kupotea na samaki kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana uharibifu mkubwa wa mazalia na uvuvi wa samaki wadogo.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке