KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 05/03/2026
MAFUNGO YA KWARESMA 2026 - SIKU YA 14
NENO KUU:
Mhubiri 3:1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
Matendo 3:19
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
MADA:
"KUTOKA MISIMU MPAKA KUSUDI" (FROM SEASONS TO REASON)
MWENDELEZO:
MISIMU & KUSUDI KATIKA MAISHA YA IBRAHIMU
(ABRAHAM'S SEASONS & REASON)
MWANZO 12:1-9
SOMO LA LEO:
UPAKO WA MAANDALIZI KATIKA MISIMU
3. KUKUGEUZA MOYO WAKO.
“Kukutengenezea sifa na tabia zinazohitajiwa na Kusudi”
1 Samwel 10 : 1 - 6
1 Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta e uwe mkuu juu ya urithi wake.
2 Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu?
3 Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai;
4 nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao.
5 Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri;
6 na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine.
1 Samwel 6 : 1, 3
1 Basi, hilo sanduku la Bwana lilikuwamo katika nchi ya Wafilisti muda wa miezi saba.
3 Nao wakajibu, Mkilirudisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe kitupu; lakini msikose kumpelekea na matoleo ya kosa; hivyo mtapona, tena mtafunuliwa ni kwa sababu gani mkono wake haukuondolewa kwenu.
Zaburi 89 : 20 - 24
20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
21 Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.
22 Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa.
23 Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia.
24 Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka.
UPAKO UNAKUTENGENEZEA SIFA ZIFUATAZO
1. Kusamehe
1 Samwel 26 : 8 - 12
2. Utayari
Matendo 13 : 36
3. Ujasiri
1 Samwel 17 : 34 - 37
4. Uaminifu
Zaburi 89 : 20 - 24
AGENDA ZA MAOMBI
1. Omba Mungu akupe upako wa kukuandaa na kukuvusha msimu uliopo ili ufikie kusudi.
2. Omba Mungu akupe upako utakaokutambulisha kwa wengine ili upate msaada kwenye msimu uliopo.
3. Omba Mungu akupake mafuta yatakaoinua watu wa msaada katika msimu unaopitia.
4. Omba Mungu akupe upako utakaokutengenezea tabia za kusudi.
Mhubiri : Mwl.Benjamin Abel.
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com
Информация по комментариям в разработке