Fafanuzi Rahisi Ya Kitabu Cha Ufunuo Wa Yohana - Sura Ya 4 (Wazee 24 na Wenye Uhai wa 4) na Askofu Dr. Fredrick Simon
MAONO YA MBINGUNI
1. PANDA HATA HUKU
4:1 “Panda hata huku”; maneno hayo yana maana kuu 2.
ii. Yohana alitakiwa apande katika ulimwengu wa kiroho, apate kuyaona mambo mengi ya mbinguni. Musa pia aliambiwa apande juu (Kutoka 19:20,24).
iii. Watakatifu wanatakiwa wapande juu kabla ya Dhiki kuu Luka 21:36; 2Wathesalonike 2”7,8. Dhiki kuu ni pigo kwa ajili ya dhambi – Sefania 1:17. Hasira ya Bwana si juu yetu sisi tuliookoka 1Wathesalonike 5:9.
2. WAZEE ISHIRINI NA NNE – 4:4,10; 5:5
Hawa ni:-
i. Wawakilishi 12 wa makabila 12 ya Israeli, huwakilisha Agano la Kale – Mwanzo 49.
Majina yao yanatajwa katika kitabu cha Hesabu 2
ii. Mitume 12 wa Yesu Kristo, wanawakilisha Agano Jipya – Ufunuo 21:10-14.
Majina yao yanatajwa katika Mathayo 10:2-4.
3. WENYE UHAI WANNE - 4:6-8.
Hao wenye uhai wanne wanaotajwa ni mfano wa Simba, Ndama na Tai, ila pia alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu. Wote hao wanamtaja Yesu Kristo kama anavyofafanuliwa katika injili zake nne, kama ifuatavyo:-
i. Mfano wa Simba (5:5) – Yaani Yesu sio mnyama simba, ila kibiblia simba humaanisha Mfalme. Hapo humaanisha kwamba Yesu Kristo ni Mfalme, na Injili pekee inayomtaja hivyo ni Injili ya Mathayo. Ndiyo maana injili ya Mathayo pekee inataja kuhusu mamajusi wa mashariki walienda wakiuliza “.... Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa wayahudi?.....” Mathayo 2:1,2.
ii. Mfano wa Ndama – Hii inawakilisha Injili ya Marko inayomtaja Yesu kama Mbeba mizigo ya watu, yaani Yesu ni Mtumishi.
iii. Uso kama wa Mwanadamu – Hii ni Injili ya Luka pekee iliyomtaja Yesu katika ukoo wa Mariamu, kuonyesha kuwa Yesu ni mwanadamu halisi. Ndio maana, uzao wa Yesu katika injili ya Mathayo, ni tofauti na jinsi ilivyotajwa katika injili ya Marko
“Kitabu cha ukoo wa Yesu mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; ...Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo” – Mathayo 1:1,2,16.
Ambapo katika Luka 3:23 tunasoma,
“Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli, wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu”.
Katika injili ya Mathayo, tunaona Yesu akitajwa katika ukoo wa Kifalme. Katika Luka Yesu anatajwa kama mwanadamu wa kawaida kabisa. Unajua kwa nini? Mathayo anamtaja Yusufu mwana wa Yakobo, ambapo Luka anamtaja Yusufu kama mwana wa Eli (Huyo Eli alikuwa ni baba mzazi wa Mariamu mama wa mwokozi wetu Yesu).
Tunaelewa wazi kwamba Yusufu sio baba mzazi wa Yesu, ndio maana Yesu Kristo hakuwahi kumwita Yusufu popote katika maandiko kwamba ni baba yake.
iv. Mfano wa Tai – Hii ni Injili ya Yohana inayomfafanua Yesu kuwa ni Tai, yaani Mungu mwenye nguvu – Yohana 1:1; 20:28.
Tunaona wazi kwamba wenye ‘uhai wanne’ ni viumbe wanaomfafanua Yesu Kristo alivyo, kulingana na Injili hizo Nne zinavyomfafanua. Hata Ezekieli aliona maono yanayofanana na hayo (Ezekieli 1:6,10).
Wenye uhai hao wanne pia ni mfano wa makundi manne katika safari ya waisraeli. Katika bendera za makundi hayo manne, zilizokuwepo picha za wenye uhai hao wanne katika kumtabiri Kristo Yesu (Hesabu 2:1-3; 10:14-28).
Mungu Akubariki Sana
Usisahau ku Subscribe, Like, Comment na ku share
#bishop #fredricksimon #UfunuowaYohana #wazee24 #wenyeuhaiwanne
#mahubiri #sikuzamwisho
Информация по комментариям в разработке