KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 09/ 07/ 2024

Описание к видео KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 09/ 07/ 2024

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 09/ 07/ 2024

SEMINA YA NENO LA MUNGU:
MADA:
"HOFU YA MABADILIKO"
(FEAR OF CHANGE)

SOMO LA LEO: VITA YA MABADILIKO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO


NENO KUU:
"UTABARIKIWA UINGIAPO, UTABARIKIWA NA UTOKAPO"
KUMBUKUMBU LA
TORATI 28 : 6
&
Yohana 12 : 24

24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.

MAANDIKO YA LEO:
Waefeso 6 : 12
Isaya 42 : 22


Waefeso 6 : 12

12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Isaya 42 : 22

22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.

3. Viwango vinavyowekwa kwenye ulimwengu wa roho vinaweza kuathiri mfumo wa fikra na muhusika ili asiwe na fikira za kimabadiliko hatakama rasilimali zote anazo.

2 Wafalme 2 : 19

19 Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.

Wagalatia 3 : 1

1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?

i. Unanyimwa maono yakinifu (Clear vision);
Maono yakinifu ni mawazo au ndoto za baadae ambazo zinamsingi wa kweli na uwezekano wa kufikiwa.

Isaya 43 : 8

8 Walete vipofu walio na macho, na viziwi walio na masikio.

Marko 8 : 18

18 Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki?

Mithali 29 : 18

18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

ii. Unanyimwa ubunifu (lack of creativity);
Ni kukosa uwezo wa kutengeneza au kuunda kitu kipya, kukosa uwezo wa kutatua changamoto kwa njia tofauti ili kuleta badiliko chanya lenye manufaa kwenye jamii au katika maisha ya watubinafsi.

Waefeso 4 : 17 - 18

17 Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao;

18 ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;

''Lengo la kumpatia mtu elimu ni ili aweze kurejea katika jamii yake na kusaidia kuondoa ujinga, maradhi na umasikini''
( Mwalimu Julius Nyerere)


iii. Ubinafsi (Selfishness);
Hali ya kua na kipaumbele cha wewe zaidi, (Roho ya Herode)

Mathayo 2 : 16

16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.

iv. Kuridhika (Contentment);
Ni hisia za kukubaliana na kutosheka na hali iliyopo bila ya kutamani mabadiliko zaidi. Huoni kupungukiwa.

Nehemia 2 : 2 - 3

2 Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana.

3 Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto?


Mhubiri: Mwnj. Paul Ringo.

Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe: [email protected]

Комментарии

Информация по комментариям в разработке