WADAU WA HAKI JINAI MKOA WA KIGOMA WASEMA OTM IMEKUWA MSAADA WA KUPUNGUZA MALALAMIKO YA WANANCHI.

Описание к видео WADAU WA HAKI JINAI MKOA WA KIGOMA WASEMA OTM IMEKUWA MSAADA WA KUPUNGUZA MALALAMIKO YA WANANCHI.

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa Mikoa ya Tanzania Bara ukiwa na ardhi yenye rutuba ya kutosha, uoto wa asili na hali ya hewa ya kuvutia. Mkoa pia unayo bionuai adimu yenye kuvutia watalii kutoka ndani na nje ya nchi. Ipo milima, mabonde, Mito na Ziwa Tanganyika ambalo linashika nafasi ya pili duniani kwa kuwa na kina kirefu cha maji. Aidha shughuli za kiuchumi katika Mkoa huo zimeendelea kuimarika kutokana na jitihada za Serikali za kuboresha huduma mbalimbali za kijamii, miundombinu ya barabara, Reli, umeme na usafiri wa anga.
Mkoa wa Kigoma kwa sasa una Wilaya 6, Halmashauri 8 (moja ya Manispaa, moja ya Mji na sita za Wilaya), Tarafa 21, Kata 136, Vijiji 306, Mitaa 176 na Vitongoji 1,856 hali hiyo unaufanya Mkoa kuwa na idadi ya watu 2,470,967 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке