NDUGULILE ATINGA BUNGENI BAADA YA USHINDI WHO, AWATAJA MAKAMBA, RAIS SAMIA KUMSAIDIA KAMPENI

Описание к видео NDUGULILE ATINGA BUNGENI BAADA YA USHINDI WHO, AWATAJA MAKAMBA, RAIS SAMIA KUMSAIDIA KAMPENI

Mteule wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dk Faustine Ndugulile amesema anatarajia kuanza kazi rasmi ifikapo Machi 2025, baada ya kupewa miezi sita kujipanga.
Dk Ndugulile amesema hayo leo Jumanne, Septemba 3, 2024 jijini Dodoma wakati akitoa salamu zake bungeni, baada ya kukaribishwa na Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu.
“Nimepewa miezi sita kujipanga, kuandaa maono yangu nitakapoanza kazi Machi mwakani, nia ya kufanya hivyo ninayo, sababu za kufanya hivyo ninazo na uwezo wa kufanya hivyo ninao.
“Niwaombe mniombee, tuendeleze sala na dua nyingi kwani nafasi hii imebeba maono ya Watanzania na Waafrika wanatarajia makubwa, kikubwa niishukuru Serikali nzima na wabunge kwa kuniunga mkono nitakuwepo katika kipindi cha mpito, napokea maoni na ushauri kutoka kwenu,” amesema Dk Ndugulile.
Dk Ndugulile anakuwa Mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo, na wa kwanza Afrika Mashariki kushika nafasi hiyo.
Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi

Комментарии

Информация по комментариям в разработке