AIC Chang'ombe Choir (CVC) - MSIKILIZE ROHO (Official Live Video)

Описание к видео AIC Chang'ombe Choir (CVC) - MSIKILIZE ROHO (Official Live Video)

#,MSIKILIZE ROHO ni wimbo wa Tisa katika IBADA YA MOYO WA SHUKRANI iliyofanyika 10 NOV, 2023 katika kanisa la AICT Chang'ombe, Sokota Temeke Dar es salaam.
Ndani ya wimbo huu AIC Chang'ombe Choir tunamshukuru Mungu kwa baraka zake alizotukirimia kwa zaidi ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa kwaya yetu.
Tunaamini wimbo huu utaenda kukusaidia kuisikia sauti ya MUNGU. MUNGU AKUBARIKI.

LYRICS

MSIKILIZE ROHO
Msikilize Roho wa MUNGU
Anavyo fundisha
Roho wa MUNGU ufundisha unyenyekevu
Roho wa MUNGU ufundisha kuwa na hekima
Upole, uelekevu, kutenda mema
Uvumilivu, kuishinda dhambi
Kushukuru kwa kila jambo
Kuwa samehe waliokukosea

Mwanadamu, mwanadamu, Mwanadamu
tembea na neema hii
Kwakuwa Muda sasa upo
YESU yupo kazini
Watenda kazi wake wapo kazini
Kungari muda sasa upo
Msikilize Roho
Msikilize MUNGU
Lisikilize neno lake
Usije shikwa na dhambi
Usije shikwa na mwovu
Usije shikwa na adui
Usije shikwa na dunia
Kungari muda sasa upo msikilize Roho
Msikilize MUNGU
Lisikilize neno lake

Kuna watu wamesahau
Kuwa MUNGU ndiye muumbaji
Wamesahau kuwa ndiye aliyeumba
Dunia na vyote
Wanatenda dhambi bila hata woga
Wamekuwa kama watu wa sodoma na gomora
Walitenda dhambi bila hata woga
Wakaiinua hasira ya MUNGU
Wakamkasirisha MUNGU
Walitenda dhambi bila hata woga

Watu wajifunze kupitia wewe MUNGU
Uinuliwe, U heshimiwe, Na usifiwe, BWANA MUNGU


Special Thanks
AICT CHANG'OMBE CHURCH
Mch. Dr Joseph Mayala Mitinje

CREDITS.
Song writer - Barthrolomew Magulu
AICT Chang'ombe Church
AIC Chang'ombe Choir (CVC)

MUSIC DEPARTMENT
Music Team - Benjamin Makolobela (MD,MAIN KEYS)
Elisha Gurlaty (AUX 1)
Elia Mahuna (AUX 3)
Onesmo Peter (AUX 2)
Nestory Ntogwa(BASS)
Jeremiah Madaha (LEAD GUITAR)
Mayala Bubele (TRUMPET)
Charles Stenson (TROMBONE)
Meshack Wilson (TROMBONE)
Eliya Makaya (ALTO SAX)
Raphael Luhende (ALTO SAX)
Samson Mathew (DRUMS)

Video production - CVC Media
Audio Mixing & Mastering Engineer - Tamie Bimha
Sound System, Backline, Lights, Stage - Haddypro Campany Limited
Project Manager - Dr.Elidady Msangi Ejazz01 Music Pro

Комментарии

Информация по комментариям в разработке