MAGARI NA ABIRIA WALIKWAMA LINDI WAANZA KURUHIWA KUENDELEA NA SAFARI

Описание к видео MAGARI NA ABIRIA WALIKWAMA LINDI WAANZA KURUHIWA KUENDELEA NA SAFARI

Magari ya Mizigo, Mabasi na magari mengine madogo yaliyokwama kwa siku sita katika barabara ya Lindi-Dar es Salaam eneo la njia nne (Mikereng’ende) hadi Somanga yakitokea Lindi kuelekea Dar es Salaam yaanza kuruhusiwa kuendelea na safari.

Hatua hiyo imechukuliwa leo asubuhi, tarehe 09 Mei, 2024 Mkoani Lindi mara baada ya kukamilisha urejeshaji wa mawasiliano katika maeneo ya Mikereng’ende, Songas na Somanga ambayo yalikatika kutokana na mvua zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.

Akisimamia zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack amewataka wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara kusafiri kwa tahadhari ambapo maeneo mengine yanaendelea na matengenezo.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке