Kauli ya RC Chalamila baada ya kufika Kariakoo, awapiga biti watakaowafanyia vurugu waliofungua

Описание к видео Kauli ya RC Chalamila baada ya kufika Kariakoo, awapiga biti watakaowafanyia vurugu waliofungua

Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wafanyabishara waliofungua maduka yao leo Jumatatu Juni 24, 2024, licha ya kuwepo kwa mgomo wa baadhi ya wafanyabishara, atalinda biashara zao na hawatafanyiwa vurugu.
RC Chalamila amesema atakayejaribu kuwafanyia vurugu wafanyabiashara waliofunga maduka yao, atashughulika naye.
“Nataka niwathibitishie yule atakayemletea mkwara aliyekubali kufungua, naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonyesha ‘show’ nzima. Kwa sababu mtu anakubali kufungua na wewe unamchimba mkwara, mimi ntakuchimba mkwara na hautainuka tena,” amesema.
Aidha, Chalamila amesema kero zilizopelekwa na wafanyabishara hao serikalini zinaendelea kushughulikiwa.
Wafanyabiashara hao wamegoma, baada ya Jumamosi Juni 22, 2024 kusambaa vipeperushi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa mgomo huo utakaoanza leo.
Wafanyabiashara hao wamefunga maduka kwa madai ya kuchoshwa na vitendo wanavyofanyiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Karikaoo, Martin Mbwana akizungumza na Mwananchi Juni 22, 2024 alikiri kuona vipeperushi hivyo, akieleza hiyo ni hasira za kuchoshwa na wanayofanyiwa na TRA.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке