KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING 01/ 07/ 2024

Описание к видео KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING 01/ 07/ 2024

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING 01/ 07/ 2024

UJUMBE WA LEO: VITA YA KESHO YAKO
[SEHEMU YA PILI]
Hagai 2 : 9
1 Samwal 18 : 6 - 9
Mithali 23 : 7
Warumi 10 : 17
Zaburi 144 : 1


Hagai 2 : 9

9 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.

1 Samwel 18 : 6 - 9

6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.

7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.

8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme?

9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.

Mithali 23 : 7

7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.

Warumi 10 : 17

17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Zaburi 144 : 1

1 Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana.

AGENDA ZA MAOMBI
1. TOBA.
2. Shukrani kwa Miezi sita 2024.
3. Omba Neema ya Mungu.
4. Omba uwepo wa Bwana uende pamoja nawe.
5. Omba Mungu akuepushe na Majaribu yasiyobeba kitu kwa ajili yako.

Mhubiri: Mwl. Eng. Googluck Mushi.

Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe: [email protected]

Комментарии

Информация по комментариям в разработке