Lesson 2: Sauti na Ala za Sauti

Описание к видео Lesson 2: Sauti na Ala za Sauti

Kipindi hiki kimefafanua kwa ubatini aina mbili za sauti za kiswahili na ala za sauti. Maelezo yametolewa kwa ufasaha na kwa lugha tutumbi sawia na picha ili kuwawezesha wanafunzi kuelewa sauti za kiswahili kwa urahisi.

SAUTI ZA KISWAHILI
Kama tulivyoeleza wali, sauti ni kipashio kidogo kabisa cha lugha kisicho na maana.
Sauti huandikwa kwa herufi ndogo kwa kutumia alama ya mkwaju/ mshazari “//” . Kwa mfano, /a/, /e/, /g/, /f/, /r/ n.k.
AINA ZA SAUTI
Kuna aina mbili kuu za sauti za Kiswahili
I) Konsonanti
II) Irabu/Vokali
Konsonanti ni sauti ambazo wakati wa kuzitamka hewa huzuiliwa katika sehemu mbalimbali kinywani. Kwa mfano, /d/, /t/, /s/, /z/ n.k.
Irabu/Vokali ni sauti ambazo hutamkwa kwa ulaini pasi na hewa kuzuiliwa kinywani. Mifano: /a/, /e/, /i/, /o/ na /u/.
ALA ZA SAUTI
Hivi ni viungo vinavyotumiwa kutamkia sauti. Kwa mfano, mdomo, meno,ufizi, kaakaa gumu, kaakaa laini, koo/koromeo n.k.
AINA ZA ALA ZA SAUTI
Kuna aina mbili kuu za ala za sauti:
i) Ala sogezi
ii) Ala tuli
Ala sogezi ni ala ambazo husongasonga/husogeasogea wakati wa kutamka sauti. Mifano ni mdomo wa chini na ulimi.
Ala tuli ni ala ambazo huwa zimetulia tu, hazisogeisogei wakati mtu anapozungumza. Mifano nzuri ni, mdomo wa juu, ufizi, meno, kaakaa gumu, kaakaa laini, koo/koromeo na pua.
MASWALI YA KUDURUSU
1. Eleza maana ya sauti
2. Taja aina mbili kuu za sauti za Kiswahili
3. Kwa kutoa mifano tofautisha kati ya konsonanti na irabu.
4. Tofautisha kati ya ala sogezi na ala tuli.
5. Taja ala zozote mbili zinazotumika kutamkia maneno yafuatayo:
i) Oa
ii) Kaa
iii) Paa

Комментарии

Информация по комментариям в разработке