Lesson 1: Vipashio vya Lugha

Описание к видео Lesson 1: Vipashio vya Lugha

Katika kipindi hiki nimefafanua kwa ufasaha maana ya vipashio vya lugha, kutaja vipashio vinne vya lugha, kueleza maana bayana na batini ya kila kipashio cha lugha na mifano ya kila kipashio cha lugha.

VIPASHIO VYA LUGHA
Vipashio vya lugha ni vipengee mbalimbali vinavyojumuishwa kujenga lugha. Kuna vipashio vine vikuu vya lugha:
i) Sauti
ii) Silabi
iii) Neno
iv) Sentensi
Sauti
Ni kipashio kidogo kabisa cha lugha ambacho hakina maana. Mifano ni /a/, /e/, /b/, /k/ n.k.
Silabi
Ni kipashio cha lugha chenye tamko moja
Ni kitamkwa katika neno. Kwa mifano, ba-ba katika neno baba au mwa-na-fu-nzi katika neno mwanafunzi.
Neno
Neno ni kipashio cha lugha kinachoundwa na mofimu moja au zaidi.
Neno ni kipashio kidogo kinachoweza kutamkwa baina ya mpumuo na ni kitu kihalisia kinachoweza kuhesabika. Mifano:
Mototo – nomino (N)
Anacheza – kitenzi (T)
Vizuri – kielezi (E)
Sentensi
Ni kipashio kikubwa zaidi cha lugha kilichokamilika kimaana na kimuundo. Mfano: Mama anapika chakula.
MASWALI YA KUDURUSU
1. Taja vipashio vinne vikuu vya lugha
2. Taja vipashio hivi vya lugha:
i) Kidogo kabisa kisicho na maana __________________
ii) Kinachotamkwa baina ya mpumuo _______________
iii) Kikubwa zaidi kilicho na maana __________________
iv) Chenye tamko moja ___________________________

Комментарии

Информация по комментариям в разработке