Gerald Asimulia Siku Yake Ya 1 Redioni "Sikuamini Nilifikiri Ruge Ananitania" SALAMA NA GERALD PT 2

Описание к видео Gerald Asimulia Siku Yake Ya 1 Redioni "Sikuamini Nilifikiri Ruge Ananitania" SALAMA NA GERALD PT 2

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support

MY COUSIN GERALD…

Gerald Hando ni mpwa ambaye kila mmoja wetu angependa awe naye, fun, happy, humorous and will tell you as it is, hanaga kona na haijalishi umri wako. Atakuambia kama ilivyo,au kukunyoshea malekezo bila kupindisha. He will tell the way it is wazungu husema. Jinsi ambavyo wewe utachukulia sasa hilo ni suala jengine.

Mchaga, mzaliwa wa Dar es Salaam, Gerald Hando ni moja ya majina yanayoheshimika kwenye upande wa watangazaji wa Radio na legacy yake si kitu ambacho kilijegwa kwa siku moja, au mwaka mmoja au baada ya kipindi kimoja. Ni kazi iliyofanywa kwa miaka kadhaa ya kulazimishwa na mwisho wa siku ikakaa mahala pake.

Gerald anakumbuka siku ya kwanza Marehemu Ruge Mutahaba alipomuambia kesho yake inabidi afanye kipindi cha asubuhi na alimpa kazi dereva wao ahakikishe Gerald anafika pale kwa muda muafaka, basi naaam Bwana dereva aliamkia dirishani mwake na katika hekaheka zake za kumuamsha ilibaki kidogo tu avunje na dirisha lenyewe. Ila mwisho wa siku iliwezekana na breki ya kwanza ilikua kwenye kahawa na tangawizi ili kumueka sawa!

Utangazaji haikua kazi ambayo ilikua kwenye rada zake cousin yangu Gerald, yeye ni mtu wa IT na yeye pia ndo alotengeneza system yote ya matangazo kwenye Radio ambayo bila ya shaka inatumika mpaka leo. Anakumbuka pia kazi yake ya kwanza ambayo ilianzia IPP Media na baada ya hapo ilikua ni kwenda mbele tu. Leo hii yeye ni mmoja wa matangazaji hodari kabisa na ambao wanalipwa vizuri zaidi kwenye Radio. Na pia tukizungumzia mapinduzi ambayo aliyafanya kwenye suala la kulipwa vizuri kutoka radio moja kwenda nyengine basi yeye pia ndo muanzilishi. Gerald alihama kutoka Radio yake pedwa ya wakati huo ya Clouds FM na kwenda kwenye Radio mpya ya EFM ambayo ndo kwanza ilikua inaanzishwa na pengine hakukua na uhakika wa waskilizaji, lakini alichukua hatua hiyo kwenye mpango ambao ulipikwa ukapikika. Hakufukiria sana na kwa mujibu wake alitaka kuondoka na watu kadhaa ambao walikua wanafanya yeye aonekane ndo nyota wa mchezo mara tu kipaza sauti kinapowaka.

Swali ni kwanini hasa aliamua hayo? Kutoka kwenye kipindi ambacho kinaskilizwa zaidi kwenye radio na kwenda kuanza upya? Hakua na woga? Nini kilimfanya awe na maamuzi haya? Majibu yote yamo kwenye maongezi haya ambayo yalijaa ukweli na uwazi mwingi. Pia tulimzungumzia Mpwa wake Marehemu Fredwa ambaye naye pia alikua mtangazaji wa Clouds FM, tulitaka kujua historia na mahusiano kati yao na kuhusu fununu za mitaani kwamba mpaka umauti unamkuta hakua na furaha.

Kazi ziko nyingi ila jinsi ambavyo unafanya kazi yako ndo alama na heshima huwa zinaachwa baada ya mmoja kufanya hilo kwa ufanisi wa hali ya juu na kwa Gerald Hando hilo ameweza kulifanya kwa utashi mkubwa. Yangu matumaini maongezi haya kama kawaida yatakufunza mawili matatu kwenye maisha yako na pengine jinsi ya kufanya maamuzi na pengine wakati gani ni sahihi kwa mmoja ‘kuanza upya’.

Tafadhali enjoy,
Love,
Salama.

SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible &...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Комментарии

Информация по комментариям в разработке