Silaa awasimamisha wapima ardhi wawili Dodoma; aeleza wanavyohonga viongozi viwannja kuficha madudu

Описание к видео Silaa awasimamisha wapima ardhi wawili Dodoma; aeleza wanavyohonga viongozi viwannja kuficha madudu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amemuagiza Katibu Mkuu Wizara yake, Mhandisi Anthony Sanga kuwasimamisha kazi wapima ardhi Enock Katete na Cleoface Ngoye kwa tuhuma za kuidhinisha na kubadilisha ramani ya eneo linalomilikiwa na Kanisa la Morovian kiwanja namba 1,2 na 3 Block T mtaa wa Itega Jijini Dodoma.

Waziri Silaa amechukua hatua hiyo Jumatatu, Novemba 27, 2023 jijini Dodoma baada ya kufika eneo la tukio na kujionea hali halisi ya eneo hilo ambalo tayari baadhi ya sehemu zake tayari zimeendelezwa na kuwa na majengo ya kisasa na hivyo kumuagiza Kamishna wa Ardhi wa jiji la Dodoma, Jabiri Singano kuwapa notice ya kuhama eneo hilo wale wote waliomilikishwa eneo hilo kimakosa.

Aidha Waziri Silaa amebainisha kuwa baadhi ya watendaji sekta ya ardhi wasiokuwa wema wamekuwa wakiwahonga baadhi ya viongozi kwa kuwapa viwanja kama kinga yao mara wanapokutwa na makosa ili hali viongozi hao wanakuwa hawana taarifa kama watendaji hao wana nia ovu.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке