SIDO ILIVYOJIPANGA KUTOA FURSA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO.

Описание к видео SIDO ILIVYOJIPANGA KUTOA FURSA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO.

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) limewataka wajasiriamali ambao hawatambuliki wafike Ofisi za SIDO kwa ajili kupewa mafunzo ambayo yatawasaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitathibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) jambo ambalo litawasaidia kupiga hatua kiuchumi.

Akizungumzia ushiriki wa maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji, amesema kuwa mwaka huu wamekuwa na washiriki wengi katika banda la SIDO tofauti na mwaka 2020.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке