NDOA ZA MITALA: JE KUNA KOSA LOLOTE KUOA WAKE WENGI? MBONA WATU WA AGANO LA KALE WALIOA WAKE WAKE?

Описание к видео NDOA ZA MITALA: JE KUNA KOSA LOLOTE KUOA WAKE WENGI? MBONA WATU WA AGANO LA KALE WALIOA WAKE WAKE?

Ndoa ya Kikristo ni ndoa ya mke mmoja na mume mmoja, na inapaswa kufungwa kwa kuzingatia sheria za kanisa, serikali na tamaduni husika. Hata hivyo, katika jamii nyingi duniani tangu zamani kumekuwepo na ndoa za mke zaidi ya mmoja.
Waafrika wengi hawaoni kwamba ni jambo geni kuingia katika ndoa za mitala. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mwanaume wa kiafrika anaweza kuoa mwanamke mwingine wakati wowote ule bila shida. Nakumbuka kanisa moja nililowahi kusali nilipokuwa kijana mdogo lilikuwa linaitwa Last Church of God, ambalo kwa lugha ya Kisukuma linajulikana kama “Bhatola Mhali” yaani “waoao wake wengi,” kanisa hili lilikuwa linahalalisha kabisa kuoa wake zaidi ya mmoja. Mwinjilisti wa kanisa hilo alikuwa na wake wawili. Kanisa hili hudai kwamba mpango wa Mungu kwa wanadamu ni kuhakikisha kwamba mwanaume anaoa wanawake wengi kwa kadri awezavyo, ikiwa tu ana uwezo wa kuwahudumia.
Hata hivyo, mpango wa Mungu haukuwa kwamba aweze kuoa wake wengi, kwani alipomuumba Adamu alimwumba na Hawa nao walikuwa wawili tu. Hata hivyo kwa sababu ya anguko la mwanadamu, kwa sababu ya dhambi mwanadamu alijitwalia wake zaidi kwa kadri alivyotaka.
Ndoa ya mitala ya kwanza katika Biblia ni ile ya Lameki katika Mwanzo 4:19 "Lameki alioa wanawake wawili." Na baadaye tunaona watu wengi muhimu katika Agano la Kale wakiwa na mitala; kwa mfano Ibrahimu, Yakobo, Daudi, Sulemani, na wengine. Katika 2 Samweli 12:8, Mungu, akizungumza kupitia nabii Nathani, alisema kwamba kama wake na masuria wa Daudi hawakutosha, naye angempa Daudi zaidi. Hii inamaanisha nini? Pia, Sulemani alikuwa na wake 700 na masuria 300. Kuna maswali ambayo pengine yangefaa kupatiwa majibu kadhaa; Kwa nini Mungu aliruhusu mitala katika Agano la Kale? Mungu anaionaje mitala leo hii? Hebu kwanza tuone ndoa kadhaa za wake wengi katika Biblia.
FUATILIA SOMO HILI.
USISAHAU PIA KUPATA KITABU CHA MAADILI YA KIKRISTO

Комментарии

Информация по комментариям в разработке