TALAKA KATIKA UKRISTO: JE KUNA KOSA LOLOTE KUTOA TALAKA KWA MWENZI AMBAYE MKO KWENYE MGOGORO HATARI?

Описание к видео TALAKA KATIKA UKRISTO: JE KUNA KOSA LOLOTE KUTOA TALAKA KWA MWENZI AMBAYE MKO KWENYE MGOGORO HATARI?

Talaka ni hati maalumu itolewayo na mahakama kwa ajili ya kubatilisha au kutangua muungano wa kindoa kati ya mwanaume na mwanamke. Kwa mujibu wa RITA Mahakama ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa talaka. Suala la talaka ni suala nyeti sana katika kanisa. Watumishi wengi wanahangaika kutatua masuala yanayohusiana na talaka.
Jamii zetu kwa miaka mingi zimekuwa na utaratibu wa kulinda ndoa zisivunjike kwa sababu zisizo na maana. Katika jamii zingine, kwa mfano watu wakifunga ndoa huenda mahali fulani na kufuri jipya na kulifunga mahali kama ishara ya kufunga ndoa hiyo, na baada ya kufunga wanatupa funguo baharini; kwa maana ya kwamba ndoa hiyo ni ya milele, hawana mpango wa kutalikiana.
Katika jamii zetu pia pale unapotokea ugomvi ambao unahatarisha kuvunjika kwa ndoa, mara nyingi viongozi wa kimila hushirikishwa ili kuweza kunusuru ndoa hiyo. Mara nyingi hujaribu kuonya upande wenye makosa. Kwa maneno mengine, jamii pia inaona kwamba talaka ni suluhisho la mwisho katika utatuzi wa masuala ya kindoa.

FUATILIA MHADHARA HUU, NA BAADAYE JITAHIDI UPATE NAKALA YA KITABU CHA MAADILI YA KIKRISTO

Комментарии

Информация по комментариям в разработке