Dakika 25 za hoja ya Mbunge Ole Sendeka, Mawaziri waingia 18 za Spika Tulia

Описание к видео Dakika 25 za hoja ya Mbunge Ole Sendeka, Mawaziri waingia 18 za Spika Tulia

Spika w Bunge, Dk Tulia Ackson ameielekeza Serikali ikafanyie kazi madai ya mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kwamba Serikali imepanga kuchukua vijiji 80 vya wafugaji wa Simajiro na vijiji vingine kadhaa vya wafugaji wa maeneo mingine kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori.

Hayo yametoke bungeni leo Jumatatu ya Juni 3, 2024 wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Spika alitoa maelekezo hayo baada ya maelekezo yake ya kwanza ya kumtuma Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, Zainabu Katimba kumtafuta Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Simanjiro, Gracian Makota ili aeleze kama aliandika barua hiyo.

“Nimepokea barua hapa kutoka kwa mheshimiwa Ole Sendeka hii barua imeandikwa na mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Simanjiro, Gracian Makota (amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro toka Agosti 2021).

“Mheshimiwa Naibu Waziri wa Tamisemi huyu bado ni mkurugenzi wa Simanjiro (sauti zikasikika ndiyo). Mheshimiwa Naibu Waziri hebu nenda hapo nje mpigie simu kuhusu hii barua.

Barua imeandikwa kwa ofisa mtednaji Kijiji cha olcholoni tarehe 16 tathmini ya maeneo yenye wanyamapori katika mapori ya Simanjiro na Berela na Simanjiro Kitiangare. Mkurugenzi akaseme aliandika hiyo barua au hapana.”

Tazama zaidi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке