KAULI YA OMO-KIU YA ACT IMEKATWA-ACT HAMNA DOGO USIFANYE JAMBO UKATAKA SIFA IJE KWAKO

Описание к видео KAULI YA OMO-KIU YA ACT IMEKATWA-ACT HAMNA DOGO USIFANYE JAMBO UKATAKA SIFA IJE KWAKO

Mhe. Omo amuaga babu Duni 04.09.04
Mkoa wa Mjini Magharibi
Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman amesema kwamba unapopigania uadilifu na haki katika nchi huwezi kuchoka iwapo jukumu hilo halijakamilika na anayechoka huwa hana tabia ya uongozi.
Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo huko ukumbi wa Majid Kiembesamaki wilaya ya Magharib Unguja alipotoa salamu katika sherehe maalum iliyofana ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Babu Juma Duni Haji.
Amesema kwamba Babu Duni amewafunza watu na viongozi wengi kwa kuwa kiongozi bora ambaye hakujenga uzio katika uongozi wake ili kuwafunza watu masuala mbali mbali na kuwataka wananchama wa chama hicho kusimama na mafunzo ya uongozi wa Babu duni ambao ni marejeo kwa wengi.
Kwa upande wake akitoa salamu zake baada ya kukabidhiwa zawadi mbali mbali kutoka kwa viongozi na wanachama wa mikoa yote ya Unguja na Pemba likiwemo gari la kifakhari aina ya Prado TZG, amesema kwamba chama hicho kimempatia heshima na bahati kubwa ambayo viongozi wenzake walioasisi kupigania mageuzi na ambao wote washatangulia mbele ya haki hakupata bahati hiyo.
Hivyo , ametoa shukrani maalum kwa viongozi na wanachama wa chama hicho na kuahidi kwamba hawezi kwenda kinyume na maelengo ya chama hicho na kwamba yupo tayari kuendelea kusaidia kutumia maarifa yake katika kukitumikia chama kupigania mageuzi ya Kidemokrasia pale atakapohitajika kufanya hivyo.
Hata hivyo, amesema kwamba anachukizwa sana na hali ya kisiasa ya Zanzibar kwamba kila kinapofika kipindi cha uchaguzi ndio kinakuwa kipindi cha sababu za machafuko, mateso kwa wananchi na watu kuawa na kujeruhiwa kutokana na siasa za kibaguzi jambo ambalo ni fedheha na aibu kwa Zanzibar.
Amehamaisha kwamba masuala ya machafuko kisiasa ni jambo linalotokea sana katika nchi mbali mbali duniani ,lakini baada ya kutokea hali hiyo watu hukaa kutafuta njia salama ili mambo kama hayo yasijrejee katika nchi zao, lakini jambo hilo inaonekana imeshindikana hapa Zanzibar.
Amesema kwamba ni muhimu kwa wazanzibari kufuata malengo na dhamira ya Karume ya kudumisha na kuendeleza umoja likiwa ndio lengo halisi la mapinduzi kwa kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na chakula, pamoja na afya bora inayotokana na mipango sahihi ya viongozi na serikali inayokuwepo madarakani.
Kwa upande wake Kiongozi wa Chama hicho Doroth Semu, amesema kwamba chama hicho kimefanya utafiti juu ya namna bora ya kuwawenzi viongozi na kwamba kimeanzisha sera rasmi ya kuhakikisha kwamba viongozi wanaenziwa kabla ya kuondoka duniani kutokana na utumishi wao kwa chama .
Amefahamisha kwamba Chama hicho kitandelea kuwaenzi kwa vitenbdo sio tu viongozi wa ngazi ya juu waliostaafu, lakini hata watumishi wa kawaida kwa kupatiwa huduma na stahiki mbali mbali ikiwemo makaazi kwa wale wasiokuwa nayo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho upande wa Zanzibar Ismail Jussa Ladhu, amesema kwamba Babu Duni amepata bahati ya heshima kubwa kwa mapenzi na imani kutoka kwa wananchama na viongozi wenzake ambayo wenzake hawakubahatika kuipata.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке