BASHUNGWA AWAKA, MKANDARASI HUYU MATATANI "ASAKWE, ALIPE, ACHUKULIWE HATUA" CRB KIBARUANI..

Описание к видео BASHUNGWA AWAKA, MKANDARASI HUYU MATATANI "ASAKWE, ALIPE, ACHUKULIWE HATUA" CRB KIBARUANI..

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amemuagiza Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) kumtafuta na kumchukulia hatua za kisheria Mkandarasi Mohammed Ally wa Kampuni ya Sure Civil and Building Contractors Company Ltd aliyetekeleza ujenzi wa majengo katika Hospitali ya wilaya Karagwe ‘Nyakanongo’ kwa kushindwa kulipa shilingi Milioni 24.7 ya vifaa vya ujenzi alivypokopa kwa mfayabiashara licha ya ujenzi huo kukamilika miaka miwili iliyopita.

Bashungwa ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Mfanyabiahara huyo, Abineza Ginivian wakati akikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mji wa Kayanga wilayani Karagwe.

Waziri Bashungwa akiongea kwa njia ya simu na Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Rhoben Nkori amemuagiza kumtafuta Mkandarasi huyo kuhakikisha analipa deni ambalo alikopa kwa mfanyabiashara huyo wakati ujenzi wa hospital ya wilaya Karagwe ukitekelezwa.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке