WANANCHI KITONGOJI CHA OLEMOOTI WAMUOMBA MWENYEKITI KUTATUA BAADHI YA KERO KABLA YA UCHAGUZI.

Описание к видео WANANCHI KITONGOJI CHA OLEMOOTI WAMUOMBA MWENYEKITI KUTATUA BAADHI YA KERO KABLA YA UCHAGUZI.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Loiborsoit A ameendelea na ziara ya kitongoji kwa kitongoji katika kijiji cha loiborsoit A, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Akizungumza katika kitongoji cha lemooti Mwenyekiti huyo Lengai Saalash Amesema lengo la ziara hiyo ni kuyatathimini , kuyaeleza, kubainisha miradi yote iliyotekelezwa ndani ya uongozi wake kwa miaka 5 katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Pamoja na hayo mh Lengai amepata nafasi ya kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wananchi wa kitongoji hicho ikiwemo kero ya barabara, umeme, maji, pamoja na kuomba kupatiwa suluhu ya mgogoro baina yao na mwekezaji aliyepo katika eneo hilo, Ambapo Majibu ya kero hizo zilijibiwa na mwenyekiti huyo papo hapo.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке