AJENGA NYUMBA YA KISASA MADALE BAADA YA KULIPWA FIDIA YA BONDE LA MSIMBAZI

Описание к видео AJENGA NYUMBA YA KISASA MADALE BAADA YA KULIPWA FIDIA YA BONDE LA MSIMBAZI

AJENGA NYUMBA YA KISASA
MADALE BAADA YA
KULIPWA FIDIA YA BONDE
LA MSIMBAZI
Mwanzoni nilipojenga hapa hapakua na shida yoyote kulikuwa na eneo kubwa la wazi, lakini miaka ilipozidi kwenda mji mji ukakua na watu wakajenga na kuzuia mitaro ya maji.

Miaka ilipozidi kwenda mvua zikinyesha kwa wingi maji yakaanza kujaa na kutufikia wakaazi wa msimbazi kutokana na njia za maji kuziba kwa sababu watu wakikuwa wanatupa taka na kujenga bila mpangilio.

Mradi huu tumeupokea vizuri sana kwakua wengi tumeshachoshwa na adha ya mafuriko kila wakati ambayo yakitupa mahangaiko sana na wengine walihama kabisa kutokana ba kupigwa na mafuriko. Sasa tutatoka hapa kwenda sehemu nyingine salama na maisha yataendelea.

Ninashukuru sana fidia nimepokea na nimesaini tayari nimeanza kujenga makazi yangu mapya Madale, nimejenga nyumba nzuri ya kisasa ambayo notábamos ikikamilika. Kwa ujumla mradi ni mzuri kwa sababu umetusaidia, sasa tunaishi pakavu, pazuri, hewa ni safi kwa kweli tunamshukuru sana Mama Samia kwa alichotufanyia.

Matarajio yangu kuwa kuanza kwa mradi mpaka kumalizika zitazaliwa ajira nyingi kwa vijana wa kitanzania, na pia ukimalizika fursa zitakua nyingi sana hivyo ninamatarajio makubwa sana na mradi huu.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке