NJIA RAHISI YA KUPATA VIFARANGA WENGI WA KUKU WA KIENYEJI 2021

Описание к видео NJIA RAHISI YA KUPATA VIFARANGA WENGI WA KUKU WA KIENYEJI 2021

Njia rahisi ya kupata vifaranga wengi wa kienyeji kwa muda mfupi.

Katika mfululizo wa vipindi vyetu vya ufugaji wa kuku, tunahitaji kumuinua mfugaji wa kuku wa kienyeji aache kuishi na kuku na aanze kufuga kuku wa kienyeji kibiashara. Ili ufuge kuku wa kienyeji kibiashara unatakiwa kuwa na makoo yasiyopungua 250. Sio rahisi kwa Wafugaji wa kuku wa kienyeji kuwa na mtaji mkubwa kiasi hicho.

Ili Kujifunza zaidi tafadhali tazama video hii
   • ULEAJI WA VIFARANGA WA KIENYEJI KWA N...  

Kufanikisha zoezi hili mfugaji anapaswa kuandaa vitu vifuatavyo:-
1. Banda bora na litakalo endana na idadi ya kuku anaohitaji kufuga.
2. Makoo 20 na jogoo 3 - 4 (Makoo ni kuku ambao wametaga angalau mara moja). Makoo watasaidia kupunguza muda wa kusubiri ili kuliona yai la kwanza.
3. Vifaa vya maji, chakula, joto na bruda
4. Chumba maalumu cha kulelea vifaranga
5. Makasha ya kutunzia mayai
6. Elimu ya ufugaji bora wa kuku, itasaidia kutatua changamoto mbalimbali za mradi wako

Hatua 1;
Nunua koo 20 na jogoo 3 - 4 kutoka kwa Wafugaji unao wafahamu. Jitahidi kununua hao kuku kutoka sehemu tofautitofauti ili kuepuka magonjwa ya kurithi kizazi hadi kizazi.
Chagua koo na jogoo wenye maumbo makubwa na wenye afya ili kupata mbegu bora na inayokuwa haraka.
Ukiwafikisha bandani, wape antibiotics kwa siku 5 kwaajili ya tahadhari ya magonjwa ya bakteria. Wasipo onyesha ugonjwa wowote, wape chanjo ya kideri/Mdondo (Newcastle disease Vaccine) na utunze kumbukumbu kwaajili ya kurudia chanjo hiyo kila baada ya miezi 3.

Hatua 2;
Watenge hao kuku katika ratio ya 1:6 au 1:7, yani jogoo 1 na majike 6 au 7 ili kuwa na urutubishaji mzuri wa mayai yatakayokupa vifaranga wengi na wenye ubora. Pia kuwatenga kila jogoo na Koo wake katasaidia kupunguza majogoo kupigana na kuwafanya warutubishe mayai vizuri.

Hatua3;
Baada ya wiki 2 - 3 kuku wataanza kutaga. Nunua mayai ya kisasa na uyawekee alama kisha uyaweke kwenye viota na kila siku kuku anapotaga yai, lichukue kisha liandike tarehe ya kutagwa na ulihifadhi kwenye makasha uliyoyaandaa.
Zingatia kuweka mayai 2 ya kisasa kwenye kila kiota cha kuku anaetaga.
Fanya hivyo kwa kila kuku atakae taga.

Uhifadhi wa Mayai
I. Mayai yahifadhi kwenye makasha ya boksi (trays) huku sehemu ya yai iliyochongoka ikiwa Chini na sehemu ya duara ilkiwa juu.
II. Mayai yahifadhiwa kwa mstari kufatisha siku ambayo yai lilitagwa.
III. Yahifadhi sehemu yenye mwanga hafifu, Joto la kawaida la chumba (Room temperature 25°C) na hewa ya kutosha ili yasiharibike. Maranyingi tunahifadhi chini ya uvungu wa kitanda (Zingatia usafi wa chumba)
IV. Mayai kwaajili ya kuatamiza hayatakiwi kuzidisha Siku 14 kabla ya kuatamiwa. Mfano kuku akitaga mayai 16, mtolee mayai mawili ya kwanza kutagwa kwa sababu yatakuwa yamezidisha siku 14.

Hatua 4;
Baada ya muda wa siku kadhaa kuku wataanza kuatamia, waachie yale mayai ya kisasa tuliyoyaweka mwanzo wa yaatamie tukisubiri idadi ya kuku wanaotaka kuatamia ifike 14 -15.
Wakifika kuku 14 - 15 wanaotaka kuatamia, muda wa usiku kama saa 1 au saa 2 hivi, ingia bandani na mayai tuliyoyatunza awali.
Ondoa mayai yote ya kisasa na umuwekee kila kuku mayai 14 - 15 ambayo hayajazidisha siku 14 tangu yatagwe. Siku hii tutaihesabu kama ni siku ya kwanza ya mayai yetu kuatamiwa.
Kwa maana hiyo tutakuwa tumeatamiza mayai
196 - 225, ambayo yakitotoka kwa 90% tunatarajia vifaranga 176 - 200 baada ya siku 21.

Uchaguzi wa Mayai Bora ya Kuatamisha
I. Mayai yawe yamerutubishwa na jogoo (zingatia uwiano 1:6 au 1:7)
II. Chagua Mayai yenye ukubwa wa wastani, mayai makubwa au madogo kuliko wastani hayatoi kifaranga
III. Chagua mayai masafi, yasiyokuwa na kinyesi au damu na yasiwe na nyufa
IV. Chagua mayai yenye umbo la kawaida ( Oval shape), mayai ya duara au yaliyochongoka kuliko kawaida hayatoi kifaranga.

Hatua 5;
Wiki moja kabla ya kupokea vifaranga, andaa chumba cha kulelea vifaranga.
Kisafishe vizuri na kisha pulizia dawa ya kuua vimelea vya magonjwa kwa kutumia disfectant ( V-rid au D4) ili kuzuia magonjwa nyemelezi kwa vifaranga wako.
Andaa bruda na vifaa vingine vya kulelea vifaranga kama jiko au chungu cha joto, mkaa, magazeti na matandiko (maranda au pumba ngumu ya mpunga)
Andaa chakula, antibiotics na vitamin za kuwaanzishia vifaranga

Hatua 6;
Baada ya siku 21, kuku wote walioatamia watatotoa vifaranga na kama urutubishaji wa mayai ulikuwa mzuri utapata vifaranga 170 - 200.

Baada ya kusikia sauti za vifaranga, pasha joto chumba ulichoandaa hatua ya 5 masaa 4-6 kabla ya kuingiza vifaranga. Hii itawafanya vifaranga wahisi joto kama wako na mama yao (zingatia joto kama tulivyoeleza kwenye kitabu hiki).
Ingiza vifaranga kwenye bruda baada kupata joto na taratibu zingine za uleaji wa vifaranga ziendelee kama kitabu hiki kinavyoeleza.
Usisubiri kuku atoe vifaranga mwenyewe ndio umnyang'anye, atasumbua kutafuta vifaranga vyake. Pia unaweza kumpatia mayai mengine aatamie ili upate vifaranga wengine baada ya siku 21.
Ukifanya hivyo wape chakula cha kutosha na maji safi na salama.

#ufugajiwakukuwakienyeji

Комментарии

Информация по комментариям в разработке