TUKIFANYA HIVI TUTAPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA VIFO VYA WATOTO WACHANGA - DKT.RASHIDI MFAUME.

Описание к видео TUKIFANYA HIVI TUTAPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA VIFO VYA WATOTO WACHANGA - DKT.RASHIDI MFAUME.

Waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa Njombe wameshauriwa kuiga mfano kwa kuweka kitengo maalum cha huduma kwa watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) katika hospitali za Wilaya kama ilivyo katika hospitali ya Mji Njombe (Kibena), ili kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Ushauri huo umetolewa Julai 1,2024 na Mkurugenzi wa huduma za Afya lishe na Ustawi wa Jamii akiwa ameambatana na timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) iliyofika hospitali mji wa Njombe(Kibena) ,kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya nakuona uwepo wa vyumba maalum vyenye vifaa vya kisasa kwa ajili yakuwahudumia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) na changamoto nyingine za afya.

Kitengo cha kuhudumia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) kipo ndani ya jengo la mama na mtoto lililojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 173.3 ,fedha iliuojumuisha michango ya wananchi ,fedha kutoka TASAF, fedha za mapato ya ndani na michango ya wadau wa maendeleo.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке