1. MAOMBI YA TOBA NA REHEMA YA NYUMBA YA BABA YAKO - MWL. ISAAC JAVAN - (Prayer Points)

Описание к видео 1. MAOMBI YA TOBA NA REHEMA YA NYUMBA YA BABA YAKO - MWL. ISAAC JAVAN - (Prayer Points)

MAELEKEZO
Kabla hujafanya maombi haya, hakikisha umepata nafasi ya kusikiliza kwanza mafundisho yake, ambayo ndani yake yamebeba maarifa na maelekezo. Kama bado, fungua link hii    • 1. MAOMBI YA KUSHINDA VITA YA NYUMBA ...   ili kupata mafundisho haya. Ni muhimu sana usikilize mafundisho kwanza, ili utakapoanza kuomba maombi haya, yakupe matokeo mazuri katika uliwengu wa roho.

Huu ni muongozo wa maombi ya toba na rehema, yanayohusu nyumba ya baba zetu. Matatizo yanayotoka kwenye msingi wa nyumba ya baba, yanakuwa na uhalali wa kisheria, unaoyapa kibali cha kuendelea kukaa na kutesa vizazi vingi. Na kwa sababu hiyo, hayawezi kuondoka kwa kukemea peke yake. Yanahitaji maombi ya toba na rehema. Kazi ya maombi haya ni kuondoa adhabu na madhara ya kiroho yaliyopata uhalali wa kukaa ndani ya mtu, familia, au ukoo. Kwa hiyo, unapoomba maombi haya, omba kwa imani ukimaanisha. Inawezekana kabisa, makosa hayakufanywa na wewe lakini yalifanywa na baba aliyekuzaa au baba waliokutangulia.Wewe omba, halafu Mungu anaenda kufanya kitu kwa ajili yako. Kumbuka, maombi ya toba na rehema yanaondoa adhabu ya kiroho na yanafuta uhalali wa kisheria ambao shetani anausimamia.

Mungu akubariki na kukutia nguvu unapofanya maombi haya. Amen.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке