MAOMBI YA KUMFUNGUA MUME WAKO - MWL. ISAAC JAVAN

Описание к видео MAOMBI YA KUMFUNGUA MUME WAKO - MWL. ISAAC JAVAN

Haya ni maombi maalum kwa mwanamke aliyeolewa ambaye anapitia mambo yafuatayo:-
1. Mume wake ana mahusiano nje ya ndoa.
2. Mume wake ametelekeza familia.
3. Mume wake ametoka kwenye nafasi yake kama mume na kama baba wa familia.

Lengo la maombi haya ni kufungua vifungo vya kiroho ambavyo nyuma yake kuna mtu au watu. Mungu anapotaka kufanya jambo kwenye maisha, anatumia mtu. Shetani pia anapotaka kuharibu jambo, anatumia mtu. Kuna mtu au watu ambao shetani anawatumia kuharibu ndoa. Zipo ndoa zilizovunjika kwa sababu ya watu ambao shetani aliwatumia. Zipo familia zilizopoteza muelekeo na maono ya ki-Mungu kwa sababu kuna mtu au watu waliotumiwa na shetani kupitisha uharibifu. Ni maombi yetu ya kwamba maombi haya yafanyike msaada kwako, na Mungu aliye hai, kwa jina la YESU afanye urejesho kwenye ndoa yako.

Unapofanya maombi haya, simamia mstari huu, "Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe" [MARKO 10:9].

MUHIMU!
Usiombe maombi haya kwa mazoea! Omba kwa kumaanisha. Pata eneo lenye utulivu, paza sauti yako mbele za BWANA. Haya ni maombi ya vita, kwa hiyo omba kwa kumaanisha, usikae kimya katikati ya maombi. Hakikisha unapambana kwa ajili ya mume wako. Ukiona machozi yanatoka, usizuie, endelea. Mahali pa kukemea, kemea. Mahali pa kuamuru, amuru. Mungu anaenda kufanya kitu kikubwa kwa utukufu wa jina lake.

Mungu akubariki. Mshirikishe na mwanamke mwingine ambaye anaweza akanufaika na maombi haya.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке