"Swedy Mwinyi tulimtafutia mchumba akamkataa, alipenda kazi kuliko maisha yake" Mayalla afichua siri

Описание к видео "Swedy Mwinyi tulimtafutia mchumba akamkataa, alipenda kazi kuliko maisha yake" Mayalla afichua siri

Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika La Utangazaji Tanzania (TBC), Swedy Mwinyi umezikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam huku wadau wakimkumbuka kwa mengi ikiwemo ushindi wa mabao 5-0, ilioupata Simba dhidi ya watani zao Yanga, mechi iliyopigwa Mei 6, 2012.

Pascal Mayalla ambaye waliajiriwa pamoja kwa mara ya kwanza Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadaye Shirika La Utangazaji Tanzania (TBC), amesema anamtambua Swedy kama mmoja wa waliokuwa wafanyakazi bora na rafiki wa kweli aliowahi kufanya nao kazi katika kipindi chake huku akikumbushia walipomtafutia mchumba wa kuoa na marehemu akamkataa.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке