Fid Q feat Gifted - Glory (Lyric Video )

Описание к видео Fid Q feat Gifted - Glory (Lyric Video )

Glory Lyrics

Fid Q

Nilikua kama DIRA.. sina kazi baada ya chombo kutia nanga/
au kama TIBA.. sikuwa na mchongo baada ya mgonjwa kukata kamba/
MSHUMAA uliozimwa baada ya machweo kutanda/
SHUJAA aliyeminywa.. wenye vyeo waweze tamba..
nilitupwa kama pingu ya mfungwa alityetoka jela/
Au fimbo ya kipofu baada ya mpofu kuiona hela/ au mkono wa mzazi baada ya mtoto kujua kutembea/
Nilisuswa kama boya mbele ya wajuaji wa kuogelea/
nilishiwdwa kila vita.. nilipigika kama mjinga/
Sikuwahi kuamini, kuna siku na Mimi wataanita bingwa/
Wenzangu ikaanza kuwalipa.. mbona kwangu miamala haisomi? /
Nikaumiza kichwa ili mipango isigome/

Wakiweka milima Mimi ninaigeuza vitonga/
Hata nusu hatua ni hatua.. mdogo mdogo nikawa ninasonga/
Japo ni kwa mwendo wa kinyonga/
Mbegu ili kuchipua lazima ioze kwanza mjomba/
Mtaani ninakuta wana wananisemasema siwezi/
Ndani yangu ninasikia sauti inaniambia jamaa unaweza
Anguko lina herufi sita, MUAMKO linazo pia/
Huzuni ina herufi sita.. FURAHA inazo pia..

Hook:
Gifted:

Utukufu ni wako baba..Sifa zote unastahili/
Sio leo tu, hata jana.. umeonyesha unanipenda mimi


Verse 2:
Fid Q:
Niilijihisi kama.. koroboi lilozimwa mida ya machweo/
Fukofuko lilotoswa kiwavi ageuke kipepeo/
Maswali yaliyokwisha baada ya elimu kupatikana/
Sikujua. mapito niliyopita ni kipimo cha uungwana/
Niliachwa kama kiota,ndege alipojua kupaa/
Mateso hayakua ajali,bali ni mzani wa ushujaa/
Nilikua ninanuka.. haukuona kinyaa/
Ulininyanyua nikanyanyuka.. sasa kila kona ninang’aa /
Niliyoyapitia yalionyesha nguvu niliyonayo/
Majaribu yakauibua ujasiri niliopewa na Mayo/
Nikawa hodari.. nikaweza kuukabili utata/
Ndoto niliyokua nayo imegeuka uhalisia sasa/
Umefanya nijiamini pasina kuweka chembe ya uoga.. nimekubali/
Nilihitaji nianguke, ili ninyanyuke nikiwa ngangari/
Nisikate tamaa au kuhofia/
KUJIKATAA ina herufi tisa.. KUJIAMINI inazo pia..


Hook:

Gifted:
Utukufu ni wako baba

Sifa zote unastahili..

Sio leo tu, hata jana.. umeonyesha unanipenda mimi

Комментарии

Информация по комментариям в разработке