KAKA MSOMALI - KUPENDA SANA NI HARAMU

Описание к видео KAKA MSOMALI - KUPENDA SANA NI HARAMU

mwaka juzi hapa 2022, zilitoka nafasi za kwenda kwenye kambi moja ya wakimbizi uko Kigoma kwaajili ya kuwashawishi wakimbizi warudi makwao.

Nafasi zilikua chache alafu ziligombaniwa kweli maana mshahara wake ulikua sio wa kitoto. Baby wangu Calvin🥰 akanipigania na mimi nikawa nimepata iyoo nafasi.

Siku ilipofika tuliondoka kwenda Kigoma, nakumbuka ilikua ni mwezi wa Tatu, na kule tulitakiwa kukaa mwezi tu.

Hao mpaka Kigoma, tulifika salama salmini! Tulipokelewa vizuri, tukapewa msosi pamoja na malazi!Baada ya kupumzika, kesho yake ndo kazi iliyo tupeleka kule ikaanza.

Sikujua kama huku ntakutana na mkaka msomali ambaye aniliingiza kwenye matatizo ya mapenzi.

#simulizi
#lucas
#lumbasi

Комментарии

Информация по комментариям в разработке