NAIBU WAZIRI KASEKENYA AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI UKANDA WA BAHARI YA HINDI

Описание к видео NAIBU WAZIRI KASEKENYA AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI UKANDA WA BAHARI YA HINDI

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi, Godfrey Kasekenya ametoa rai kwa watanzania kuwekeza kikamilifu katika maeneo yenye uwekezaji mkubwa wa miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara hususan ukanda wa bahari ya Hindi katika mikoa ya Tanga na Pwani.

Rai hiyo ameitoa Septemba 18, 2024 alipokagua ujenzi wa barabara ya Tanga- Pangani-Saadani-Bagamoyo hadi Dar es salam (sehemu ya Tungamaa-Mkwaja-Mkange (Km 95.2) na kusisitiza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua uchumi wa Tanzania kutokana na vivutio vilivyopo katika ukanda huo hivyo ni vyema wananchi wakachangamkia fursa mapema wakati ujenzi ukiendelea.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке