SERIKALI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI KATIKA MAJIJI MATANO NCHINI, MIZANI 78 YAWEKWA BARABARANI

Описание к видео SERIKALI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI KATIKA MAJIJI MATANO NCHINI, MIZANI 78 YAWEKWA BARABARANI

Serikali imesema jumla ya mizani 78 zimefungwa nchini kwa ajili ya kudhibiti uzito wa magari ili kuzilinda barabara ambazo hugharimu fedha nyingi katika ujenzi wake.

Ameyasema hayo leo Agosti 27,2024 Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi Mhandisi, Kashinde Musa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wao kwenye wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Mhandisi Musa amesema kuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara lakini moja kati ya changamoto zinazoharibu barabara ni suala la magari kubeba mizigo mizito zaidi ya uwezo wa barabara.

#wizarayaujenzi

Комментарии

Информация по комментариям в разработке