36. MAOMBI YA KUPONYA HISTORIA YA MAISHA YAKO | MWL. ISAAC JAVAN

Описание к видео 36. MAOMBI YA KUPONYA HISTORIA YA MAISHA YAKO | MWL. ISAAC JAVAN

Hili ni somo na maombi ya kufunguliwa kutoka kwenye vifungo ambavyo vina msingi wa historia. Lengo la somo hili, ni kushughulikia vyanzo vya matatizo. Lakini pia, Roho Mtakatifu anaenda kushughulikia matatizo ambayo hayasikiagi maombi ya kawaida (matatizo sugu). Kwa hiyo, hili ni somo muhimu sana kwa watu wote, wakubwa kwa wadogo; na wazee kwa vijana.

Historia ya maisha yako, ndiyo inakufanya uwe jinsi ulivyo leo. Aina ya maisha uliyonayo, ni matokeo ya historia ya maisha yako. Hali yako kiroho, ni matokeo ya historia yako. Kwa hiyo historia ya maisha yako ikipona, maisha yako yote yanapona. Napenda kukutia moyo, usikose kufuatilia muendelezo wa somo hili pamoja na maombi yake.

Sikiliza mafundisho haya kwa utulivu na umakini mkubwa, na uelewe vizuri, ili wakati wa maombi unapofika, uweze kufanya maombi yenye faida na matokeo mazuri. Kumbuka jambo hili mpendwa katika KRISTO YESU, nguvu ya maombi yako inategemea kiwango chako cha kulielewa neno la Mungu linalogusa shida uliyonayo. Mungu analiangalia neno ili alitimize. Hivyo basi, hakikisha unalielewa neno, likupe maarifa, ili ukiomba upate ushindi kwa Jina la YESU na kwa damu ya YESU.

Mungu akubariki na kukupa ushindi daima. Amen!

Комментарии

Информация по комментариям в разработке