Nifanye Nini Nipate Kuokoka? | Kuamini na Kuzaliwa Upya | Mada ktk Injili ya Yohana | 26/12/2024

Описание к видео Nifanye Nini Nipate Kuokoka? | Kuamini na Kuzaliwa Upya | Mada ktk Injili ya Yohana | 26/12/2024

Soma Yohana 1:12, 13. Ni hatua gani zilizoelezewa hapa zinazohusu kuwa Mkristo?

Yohana aliandika Injili yake ili tuweze kumwamini Yesu na kwamba kwa kuamini tuweze kuwa na uzima wa milele katika jina Lake (Yohana 20:31). Katika Yohana 1:12, 13, mchakato huu umeelezwa katika hatua mbili. Kwanza, tunampokea Yeye, yaani, tunamwamini Yeye. Pili, Yeye anatupatia mamlaka au uwezo wa kuwa watoto wa Mungu, unaofafanuliwa katika mstari wa 13 kama aliyezaliwa na Mungu. Kwa hiyo, kuna kipengele cha kibinadamu na cha kiungu cha kuwa Mkristo. Ni lazima tutende kwa imani, tumpokee, na tuwe wazi kwa nuru, lakini yeye ndiye anayehuisha moyo.

Kwa kweli, imani yenyewe ni zawadi ya Mungu ambayo huja kwa kusikia Neno Lake (Rum. 10:17), “Ili kuwa na imani ya kweli, yenye kudumu katika Kristo, ni lazima tumjue Yeye jinsi Anavyowakilishwa katika neno.” — Ellen G. White, Fundamentals of Chrishan Education, uk. 433. “Roho akitenda kazi juu yake na kutia nuru akili ya mwanadamu, hujenga imani katika Mungu.” — Maoni ya Ellen G. White, The Seventh-day Adventist Bible Commentary, juz. 7, uk. 940.

Wale wanaomwamini au kumkubali Mwana kama Masihi wanapokea uzima wa milele. Yohana pia anasisitiza kukubali au kuamini Neno hilo ambalo Yesu alilisema ( Yohana 5:24, 38, 47). Ni kazi ya Roho Mtakatifu kuleta usadikisho ( Yn. 16:7, 8; linganisha na Rum. 8:16 ).

Soma Warumi 8:16. Ni kanuni gani kuhusu wokovu katika Yesu inayoonekana hapa?

Imani, imani ya kibiblia, yenye msingi wake katika kazi ya Roho Mtakatifu mioyoni mwetu, ndiyo msingi wa imani yetu;

“Imani ni.... baraka iliyo kuu - jicho linaloona, sikio linalosikia.” — Ellen G. White, In Heavenly Places, uk. 104. Mtazamo wa kibinadamu kwa suala la imani unasema kwamba ni lazima tupate msingi kwanza, vigezo vinavyothibitisha uwepo wa imani, ndipo tuamini. Kinyume chake, mtazamo wa kibiblia unasema kwamba imani ni msingi, karama itokayo kwa Mungu (Efe. 2:8, 1 Kor. 1:17 - 24; 1 Kor. 2:1-6). Tunaanza na msingi wa imani, kisha kuanzia hapo tunakua katika ufahamu na neema.

Ikiwa mtu atakuuliza kuwa imani yako msingi wake upo katika nini, utajibuje?

Комментарии

Информация по комментариям в разработке