Najengaje Imani ktkt ya Mashaka? | Kukataa Chimbuko la Uhai | Mada ktk Injili ya Yohana | 27/12/2024

Описание к видео Najengaje Imani ktkt ya Mashaka? | Kukataa Chimbuko la Uhai | Mada ktk Injili ya Yohana | 27/12/2024

Baadhi ya taarifa zinazosikitisha sana katika Maandiko yote zinatokea kwenye Injili ya Yohana. “Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.... (Nuru) Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua . Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea” (Yohana 1:5, 10, 11). “MIMI NIKO” alikataliwa na wengi wa watu Wake Mwenyewe.

Haishangazi kwamba baadaye Paulo anaonya, “Basi msiutupe ujasiri wenu” (Ebr. 10:35). Kama ambavyo tumeona tena na tena, Kristo alikataliwa kwa sababu watu hawakulikubali Neno Lake.

“Namna ya kisasa ya kibinadamu ya fikra huwa inaanza na mashaka. Watu huwa wanahoji kila kitu ili wapate kujua kwamba kweli ni nini. Kile kinachostahimili moto wa udadisi wa hali ya juu ndicho wanachokikubali kama ujuzi wenye msingi imara, ambacho mtu anaweza kujenga imani yake kwacho. Baadhi yao wanatumia njia hiyo hiyo kwa Biblia, wakihoji kila kitu kutokana na mtazamo wa kisayansi, kihistoria, kisaikolojia, kifalsafa, kiakiolojia, au kijiolojia ili wapate kujua kwamba kweli ni nini katika Biblia. Mbinu hiyo yenyewe inaanza na kujenga katika kutilia mashaka ukweli wa maandiko, Kristo alihoji, “Atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? (Luka 18:8).” — E. Edward Zinke na Roland Roland Hegstad, The Certainty of the Second Coming (Hagerstown,MD: Review Herald Publishing Association 2000) uk 96

Soma Hesabu 13:23-33. Ni kitu gani kilichofanya tofauti kati ya taarifa mbili wapelelezi walizoleta kuhusu Kanaani?

Dhambi ya Waebrania walipokuwa pale Kadesh-barnea ilikuwa kutilia mashaka Neno la Mungu. Mungu alikuwa amewaelekeza wakwee na kuitwaa nchi. Wapelelezi kumi na wawili walitumwa Kanaani ili kuipeleleza nchi. Walirejea na taarifa mbili. Walio wengi walitoa taarifa hasi. Kuna majitu kwenye nchi, miji iliyozungushiwa kuta, silaha ambazo hatujapata kuziona, na majeshi yaliyofunzwa Vizuri. Tofauti na sisi, tumekuwa watumwa kwenye nchi ya Misri na hivyo tuna uzoefu mdogo tu wa kijeshi. Wapelelezi kumi walipiga kura ya Hapana " wakisimamia ushahidi mzito uliotokana na mtazamo wa kibinadamu. Wapelelezi wawili walipiga kura ya “Ndiyo” wakisimamia katika imani yao katika uwezo usio wa kawaida wa Neno la Mungu.

Tunawezaje kuepuka kufanya kosa la namna hiyo hiyo lililofanywa hapa? Wakati huo huo, tunawezaje kuepuka ujuvi, yaani kufanya jambo fulani kipumbavu lakini tukiamini kwamba tunafanya mapenzi ya Mungu na kwamba hatutashindwa?

Комментарии

Информация по комментариям в разработке