Chimbuko la Uzima: Jifunze Zaidi na Ujadili Nasi | Mada ktk Injili ya Yohana | 29/12/2024

Описание к видео Chimbuko la Uzima: Jifunze Zaidi na Ujadili Nasi | Mada ktk Injili ya Yohana | 29/12/2024

Soma Ellen G. White, “Mungu Pamoja Nasi,” uk. 7-15; “Pambano,” uk. 208-216, katika Tumaini la Vizazi Vyote.

“Kwa kujishusha kuvaa ubinadamu, Kristo alifunua tabia ambayo ni kinyume na tabia ya Shetani. Bali alijishusha sana hadi kufedheheshwa. “Tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza, akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.” Wafilipi 2:8. Kama ambavyo kuhani mkuu aliweka kando vazi lake zuri la kupendeza na kuvaa vazi jeupe la kuhani wa kawaida, ndivyo Kristo alichukua mfano wa mtumwa na akatoa dhabihu, Yeye mwenyewe kuhani, yeye mwenyewe sadaka. “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu: adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake.” Isaya 53:5.

“Kristo alitendewa stahili yetu, ili tuweze kutendewa kama anavyostahili. Alihukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu, ambazo hakuzitenda, ili tuweze kuhesabiwa haki kwa haki Yake, ambayo haikuwa haki yetu. Alikufa kifo ambacho kilikuwa stahili yetu, ili tuweze kupata uzima ambao ulikuwa ni Wake. “Kwa kupigwa Kwake sisi tumepona” —Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 25.

Masawali ya Kujadili

1. Bwana Yesu alitoa kikubwa hivyo ili kuiokoa dunia. Ni njia zipi unazofikiria kuwa ndizo njia bora zaidi za kusaidia wengine ili wapate kuiona kweli hii ya ajabu na kumjia Yeye kwa imani?

2. Ni tofauti zipi kuu katika kufanya maamuzi katika viwango vya kibinadamu kukilinganishwa na kufanya maamuzi kwa msingi wa udhihirisho wa kimbingu?

3. Mambo kama ya mantiki na urazini yanapelekanaje na uelewa wa Neno la Mungu? Tuna sababu gani za kimantiki za kuijia imani? Mambo kama utimilifu wa unabii au uzuri wa kushangaza na utata wa ulimwengu ulioumbwa vinatuelekezaje kimantiki kwa kuwepo kwa Mungu na ukweli wa mpango wa wokovu?

4. Mkiwa kwenye darasa, zungumzia jibu lako kwa ajili ya swali la mwisho somo la Jumanne. Imani yako imejengwa juu ya nini? Kama mtu angekuuliza kwa nini unamwamini Yesu na madai ya injili, ungejibuje?

Комментарии

Информация по комментариям в разработке